Generation Xix

TXT

TOURISM

NMB

TTCL

TTCL

Friday 11 January 2013

Precision kuzindua safari za Mbeya

SHIRIKA la Ndege la Precision Air linatarajia kuzindua safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kuanzia Ijumaa ijayo.
Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Songwe mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano, Linda Chiza alisema abiria wa safari hiyo, watahudumiwa na ndege aina ya ATR-72, yenye uwezo wa kubeba abiria 70.
Alisema kwa mujibu wa ratiba ya shirika, ndege hiyo itakuwa inaruka mara nne kwa wiki kwenda Mbeya na kwamba safari hizo zitaongezeka kwa kadri njia hiyo itakavyoimarika.
“Lengo ni kuwapa abiria wetu unafuu wa kuchagua muda wa kusafiri unaowafaa kulingana na ratiba zao,” alisema Linda.
“Tunajivunia kuzindua safari hii mpya kuelekea Mbeya ambayo itatuwezesha sasa kuwapatia huduma abiria kutoka Mbeya na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.  Alielezea matumaini ya shirika lake kuwa kwa kupeleka huduma hizo mkoani Mbeya, litakuwa  linarahisisha usafiri kwa watalii, wafanyabiashara na  watu wengine wanaopenda kutembelea mkoa huo wenye utajiri wa vivutio vya utalii.
Vivutio hivyo ni pamoja na  Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Ruaha na Katavi na Hifadhi nyingine nyingi za taifa.
nuhu85

Ndoto ya kufufua ATCL itimie, nchi iwe na shirika lake la ndege

KWA muda wa zaidi ya miaka 10 sasa kumekuwako na mjadala mkali juu ya hatima ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) hasa uwezekano wa kulifufua ili liweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
Mbali na mjadala ndani ya jamii kuhusu mustakabali wa ATCL, pia viongozi serikalini kwa nyakati tofauti nao wamekuwa wakitoa ahadi za kufufua na kuimarisha ATCL iweze kutoa huduma zake ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa enzi za uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere.
Ni jambo la aibu na kusikitisha kwamba kama taifa lenye rasilimali zote ambazo nchi imebarikiwa kuwa nazo, tumeshindwa kabisa kufufua ATCL na hasa pale ahadi lukuki zinapotolewa bila ya kutimizwa.
Maoni yetu leo yanazidi kusisitiza kwamba ndoto ya kufufua ATCL itimie ili tuweze kuwa na Shirika la Ndege. Tunasema hivi kwa sababu sifa ya kuwa na Shirika la Ndege ni kuwa na ndege za kutosha na kutoa huduma hiyo ya usafiri wa anga bila matatizo. Tofauti na hivyo, tutaendelea kudanganyana kwamba kuna Shirika la Ndege nchini wakati hatuna.Ndiyo maana taarifa za kwamba umoja wa wafanyabiashara wa Oman wapo katika mchakato wa kukamilisha uwekezaji wa Sh160 bilioni kwa ATCL zinaongeza matumaini kuwa huenda nchi ikarejea kuwa na Shirika la Ndege.
nuhu85

Ngono inasababisha saratani ya kizazi

UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa saratani ya shingo ya kizazi, inasababishwa pamoja na mambo mengine na ngono kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi, madaktari bingwa wa magonjwa ya maradhi hayo wamesema.
Hayo yalielezwa na daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa katika Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa.
Madaktari hao wametaja mambo mengine yanayoweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa na wapenzi wengi, kusafisha sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa mara nyingi.
Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa mwanamke kuzaa bila kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto wanne.
Dk Mwakyoma alisema saratani ya shingo ya kizazi inatokana na aina 40 ya virusi, aina mbili ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia ya ngono... “Human papilloma virus (HPV) Squamos cell carcinoma kirusi namba 16 na Adenocarcinoma namba 18, ni kati ya virusi 40 vinavyosababisha saratani ya kizazi na vyenyewe vinachangia tatizo hilo kwa asilimia 70.”
Alisema saratani ya uzazi ndiyo inayoongoza ikilinganishwa na nyingine nchini na asilimia 80 ya wagonjwa, wameambukizwa kwa ngono.
“Saratani hiyo husambaa kwa ngono kutoka mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine. Mwanamke mwenye saratani ya kizazi akifanya ngono, mwanamume huchukua virusi na kumwambukiza mwingine atakayefanya naye ngono,” alisema na kuongeza:
“Wagonjwa wengi na wale ambao tayari wana maambukizi, wamekuwa wakikutwa na virusi hawa wa aina mbili ambao wamekuwa wakienezwa zaidi kwa njia ya zinaa. Inawezekana mwanamume akawa ametoa kirusi kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.”
“Hata hivyo, kuna wanaume ambao tayari wameshakuwa na maambukizi ya HPV wanatembea na virusi, hawa tunawaita (high risk sexual male patner) wanaume hawa utakuta kila akioa mke anakufa kwa saratani ya shingo ya uzazi, lakini kamwe virusi hao hawawezi kumwathiri yeye.”
nuhu85

MCHAKATO WA KATIBA:Mtikila aibua mapya

MAKUNDI maalumu jana 10-01-2013 yaliendelea kutoa maoni yao kwenye mchakato wa Katiba Mpya, huku DP kikipendekeza Rais aapishwe baada ya siku 90 tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Mbali na maoni hayo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila, makundi mengine; wakulima, wafugaji, wanahabari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) nayo yalijitokeza kutoa moyoni. Mtikila alisema kipindi hicho cha siku 90 kitatoa fursa kwa watu wanaotaka kuwasilisha pingamizi dhidi ya ushindi wa Rais mteule kufanya hivyo, kabla ya kuapishwa.
Alisema pingamizi linaweza kufanyiwa kazi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa taifa linapata kiongozi halali mwenye ridhaa ya wananchi. “Pia tunataka kinga ya Rais ikome pale anapomaliza muda wake wa uongozi, kama alifanya makosa yoyote ya jinai aweze kushtakiwa ili kujenga nidhamu ya uongozi katika ofisi ya umma. Utaratibu wa kumwondoa madarakani uimarishwe asisubiriwe hadi amalize muda wake wa uongozi.”Alisema kuwa Katiba ya nchi inapaswa kuwa mali ya wananchi wenyewe ili watawala wasijihusishe katika kuwaundia wananchi Katiba kama ilivyo kwa mchakato unaoendelea sasa wa kupata Katiba Mpya.
story by mwananchi magazine and powered by XI

Thursday 10 January 2013

Hoja ya JK kuhusu ubunge wa Kafumu yaibua mapya

KITENDO cha Rais Jakaya Kikwete kuhoji hukumu iliyomwengua Dk Dalaly Peter Kafumu kuwa Mbunge wa Igunga, kimewakera baadhi ya wanasheria nchini ambao wameeleza kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola.Akizindua Daraja la Mbutu mkoani Tabora, Januari 7, mwaka huu, Rais Kikwete pamoja na mambo mengine, alihoji uamuzi uliomwengua katika nafasi ya ubunge Dk Kafumu kwa kigezo cha kufanya kampeni kwa kutumia ujenzi wa daraja hilo.Rais Kikwete alihoji mantiki ya uamuzi huo wakati ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mambo yaliyopo kwenye Ilani ya CCM ya2010–2015.Akizungumzia kauli hiyo, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society (TLS), Francis Stola alisema hukumu hiyo ilikuwa sahihi kwani ni makosa kwa kiongozi wa Serikali kutumia jukwaa la kampeni za kisiasa kuzungumzia masuala yanayohusu utendaji wa Serikali akisema kufanya hivyo kunaweza kutoa ushawishi kwa wapigakura na kuvuruga mwenendo wa uchaguzi by http://www.mwananchi.co.tz
powered by nuhu85