Mtuhumiwa wa kesi ya EPA Rajabu Maranda(kushoto) akiongea na simu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam janakabla ya kuingia katika chumba cha Mahakama hiyo kwa ajili yakusikiliza kesi inayomkabili
Wananchi wakipita pembeni mwa mawe yaliyowekwa katika barabara ya Mtaa wa Kiwelu katika Manispaa ya Sumbawanga kwa zaidi ya miezi mitano na hivyo kusababisha usumbufu kwa watumiaji.
Mkurugenzi wa Benchmark Ritha Paulsen akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya ziara ya Mikoani ya kutafuta wasanii wenye vipaji inayojulikana kama bongo Star search ambapo jumla ya wasanii 800 wamepatikana.Meneja Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna
Baadhi ya wanachama wa Deci wakiwa katika tawi la Morogoro jana huku ofisi zikiwa zimefungwa wakitafakari kuhusu hatma ya fedha zao walizopanda.jamani vya bure hiviiiii
Wakazi wa eneo la Matumbi Tabata jijini Dar es Salaam wakimwangalia mwendesha pikipiki aliyejeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo hilo jana. Kumekuwa na ongezeko la ajali za wapanda pikipiki kutokana na madereva wa magari kutowajali watumiaji hao wa barabara.
Watuhumiwa wa kesi ya EPA Farijala Hussein (kulia) na mshitakiwa mwenzake Ajay Somani wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana wakisubiri kuanza kusikilizwa kesi inayowakabili mahakamani hapo
Wasamalia wema wakimasaidia mpanda pikipiki (mwenye kofia), kuinua pikipiki yake baada ya kutumbukia nayo eneo la Tazara Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akikwepa gari lilikuwa likitaka kungonga.balaaaaaaa.duuuuuuu
Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, jana kabla ya akielekea nchini Botswana kwa ziara ya siku mbili ya kiserikali. Katikati ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Abbas Kandoro.