Generation Xix

TXT

TOURISM

NMB

TTCL

TTCL

Monday, 11 May 2009

mapambano dhidi ya ukimwi


Ndivyo wanavyoonekana kujadili. Hawa ni baadhi ya vijana waliopo shule za sekondari. Hapa ni Silver Sand Camping & Site ulipofanyika mkutano mkuu wa kitaifa wa kutimiza miaka 10 wa shirika lisilo la serikali la Femina Hip.

president kikwete


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz, Mh JK ni kama vile anamwambia Rais wa Burkina Faso "Muungano wetu hautatetereka, nitaulinda na kuutunza kwa kuuimarisha zaidi"kama namsikia vile........................mambo ya CCM hayo 2010 mambo yatakuaje jiulize

Ziara ya falme za kiarabu


Ziara ya Shaikh Saud bin Saqral Al Qasimi ambaye ni Naibu mtawala wa Ras al Khaiman inaweza ikafungua milango ktk suala zima la uwekezaji hapa nchini Tanzania. Ras Al Khaiman ni miongoni mwa nchi 7 zinazounda muungano wa EMIRATES. Kiuchumi jumuiya ya EMIRATES wamepiga hatua. Ni vema basi viongozi wetu wajifunze mengi toka kwa kiongozi huyo ili kuinua na hatimaye kukuza uchumi wa nchi yetu. Pengine ziara hii ni mojawapo ya matunda ya ziara za viongozi kwa nchi za kiarabu.

kutangaza vivutio Tanzania


katika kuonesha nia thabiti ya kimaendeleo Serikali ya Tanzania imedhamiria kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini. Hapa ni siku ujumbe wa Tanzania ulipokitembelea chuo kikuu cha New York kwa ajili hiyo. Timu iliongozwa na Mh. Jumanne Maghembe (Waziri wa maliasili na utalii-wa tatu toka shoto). Pia alikuwepo balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mh. Mahiga-wa nne toka kulia. ni hatua nzuri na yakupongezwa keep it up