Generation Xix

TXT

TOURISM

NMB

TTCL

TTCL

Saturday, 28 December 2013

Brandts awagomea Yanga Dar!!

KOCHA Mkuu wa Yanga Ernie Brandts, amegoma kuendelea na kazi kama alivyokubaliana na uongozi huku akisisitiza kwamba ana kikao na uongozi kuweka sawa baadhi ya mambo.Brandts ambaye yupo katika kuitumikia notisi ya siku 30 aliyopewa na uongozi wa Yanga ikiwa ni mpango wa kumuondoa katika cheo chake hicho, alishindwa kuibuka katika mazoezi ya kikosi hicho, yaliyoendelea jana Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam akimuachia msaidizi wake, Fred  Minziro.Habari ambazo Mwanaspoti, imezipata baada ya Brandts kutoonekana katika mazoezi hayo, zinadai kwamba kocha huyo alishindwa kutekeleza kwa vitendo kuendelea kukifundisha kikosi hicho, badala yake amekuwa akitaka kukutana na mabosi wa timu hiyo, kujadiliana nao jambo moja muhimu. Imeelezwa kuwa Brandts, ameona hataweza kuendelea kukifundisha kikosi hicho, baada ya kubaini kuwa kuendelea kukifundisha kikosi hicho ndani a siku 30, hakutakuwa na maana tena kutokana na tayari viongozi wa Yanga, wameonyesha nia ya kumuondoa huku wakianza taratibu mchakato wa kumsaka mrithi wake, ikiwa ni kufikia mwisho kwa utawala wa Mholanzi huyo aliyedumu kwa msimu mmoja na nusu. Habari zinasema Brandts alipanga kukutana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga jana jioni kumalizana naye ili asiendelee na majukumu yake kwa vile ameona hayatakuwa na tija katika kikosi hicho
By nuhu85

Tundaman,Alikiba na Masogange kwenda kushuti video kenya

Tundaman akitoa taharifa amesema video yake ya Msambinungwa itafanyika nchini Kenya chini ya usimamizi wa kampuni ya Pink Lab,ambao wao husambaza video wenyewe kitu ambacho ni tofauti na hapa bongo,akizungumza mwenyewe amesema amelenga zaidi kifikia wengi na kupata kitu kilicho bora zaidi na kuliteka soko la africa akizungumza'Nataka kufika mbali kimziki'
By nuhu85

Waliochaguliwa kidato cha kwanza watangazwa

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2014. Kushoto ni Naibu wake, Zuberi Samataba.
IDADI ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani umeongezeka kwa asilimia 31.37, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 19.
Hayo yalielezwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, wakati akitangaza wanafunzi waliomaliza darasa la saba ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Januari mwakani.
Hata hivyo wakati idadi hiyo, ikifanikiwa kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wanafunzi 13 matokeo yao yamefutwa kutokana na kubainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo kumaliza elimu ya msingi mwaka huu.
Kuhusu ufaulu kuongezeka Sagini alisema kwa asilimia 19 kutokana na watahiniwa 844,938 sawa na asimilia 97.34 waliofanya mtihani huo.
Alisema kati ya hao wasichana walikuwa 446,115 sawa
na asilimia 97.85 wakati wavulana ni 398,823 sawa na
96.78.Wanafunzi  23,045 sawa na asilimia 2.66 hawakufanya mtihani kwa sabanu mbalimbali ikiwemo ugonjwa, vifo na utoro.
"Matokeo hayo ya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi yanaonesha alama ya juu ufaulu kwa wavulana ni 244 na wasichana ni 241 kati ya 250," alisema.
Aliongeza kutokana na ongezeko hilo la ufaulu wanafunzi
411,127 kati ya 427,609 waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Serikali katika awamu ya kwanza ikiwa ni sawa na asilimia 96.15.
Alifafanua wanafunzi hao waliochaguliwa wasichana ni  201,021 na wavulana wakiwa 210, 106 huku akifafanua kuwa wanafunzi 6,482 ambao wamekosa nafasi awamu ya kwanza halmashauri zimetakiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 412 ili kufanikisha wanafunzi hao kujiunga na elimu ya sekondari kuanzia Februar na Machi mwakani.
Alitumia nafasi hiyo, kuitaja mikoa ambayo wanafunzi wake wamekosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ni  Morogoro wanafunzi 315, Katavi 261, Dar es Salaam 11, 796,  Dodoma 549, Mtwara 120, Mbeya 1484 na Geita 1578.
by nuhu85