KOCHA
Mkuu wa Yanga Ernie Brandts, amegoma kuendelea na kazi kama
alivyokubaliana na uongozi huku akisisitiza kwamba ana kikao na uongozi
kuweka sawa baadhi ya mambo.Brandts ambaye yupo katika
kuitumikia notisi ya siku 30 aliyopewa na uongozi wa Yanga ikiwa ni
mpango wa kumuondoa katika cheo chake hicho, alishindwa kuibuka katika
mazoezi ya kikosi hicho, yaliyoendelea jana Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja
wa Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam akimuachia msaidizi wake, Fred
Minziro.Habari ambazo Mwanaspoti,
imezipata baada ya Brandts kutoonekana katika mazoezi hayo, zinadai
kwamba kocha huyo alishindwa kutekeleza kwa vitendo kuendelea
kukifundisha kikosi hicho, badala yake amekuwa akitaka kukutana na
mabosi wa timu hiyo, kujadiliana nao jambo moja muhimu. Imeelezwa kuwa Brandts, ameona
hataweza kuendelea kukifundisha kikosi hicho, baada ya kubaini kuwa
kuendelea kukifundisha kikosi hicho ndani a siku 30, hakutakuwa na maana
tena kutokana na tayari viongozi wa Yanga, wameonyesha nia ya kumuondoa
huku wakianza taratibu mchakato wa kumsaka mrithi wake, ikiwa ni
kufikia mwisho kwa utawala wa Mholanzi huyo aliyedumu kwa msimu mmoja na
nusu. Habari zinasema Brandts alipanga
kukutana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga jana jioni
kumalizana naye ili asiendelee na majukumu yake kwa vile ameona
hayatakuwa na tija katika kikosi hicho
No comments:
Post a Comment