IDADI ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani umeongezeka kwa asilimia 31.37, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 19.
Hayo yalielezwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, wakati akitangaza wanafunzi waliomaliza darasa la saba ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Januari mwakani.
Hata hivyo wakati idadi hiyo, ikifanikiwa kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wanafunzi 13 matokeo yao yamefutwa kutokana na kubainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo kumaliza elimu ya msingi mwaka huu.
Kuhusu ufaulu kuongezeka Sagini alisema kwa asilimia 19 kutokana na watahiniwa 844,938 sawa na asimilia 97.34 waliofanya mtihani huo.
Alisema kati ya hao wasichana walikuwa 446,115 sawa
na asilimia 97.85 wakati wavulana ni 398,823 sawa na
96.78.Wanafunzi 23,045 sawa na asilimia 2.66 hawakufanya mtihani kwa sabanu mbalimbali ikiwemo ugonjwa, vifo na utoro.
"Matokeo hayo ya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi yanaonesha alama ya juu ufaulu kwa wavulana ni 244 na wasichana ni 241 kati ya 250," alisema.
411,127 kati ya 427,609 waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Serikali katika awamu ya kwanza ikiwa ni sawa na asilimia 96.15.
Alifafanua wanafunzi hao waliochaguliwa wasichana ni 201,021 na wavulana wakiwa 210, 106 huku akifafanua kuwa wanafunzi 6,482 ambao wamekosa nafasi awamu ya kwanza halmashauri zimetakiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 412 ili kufanikisha wanafunzi hao kujiunga na elimu ya sekondari kuanzia Februar na Machi mwakani.
Alitumia nafasi hiyo, kuitaja mikoa ambayo wanafunzi wake wamekosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ni Morogoro wanafunzi 315, Katavi 261, Dar es Salaam 11, 796, Dodoma 549, Mtwara 120, Mbeya 1484 na Geita 1578.
No comments:
Post a Comment