KITENDO cha Rais Jakaya Kikwete kuhoji hukumu iliyomwengua Dk
Dalaly Peter Kafumu kuwa Mbunge wa Igunga, kimewakera baadhi ya
wanasheria nchini ambao wameeleza kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa
mhimili mwingine wa dola.Akizindua Daraja la Mbutu mkoani Tabora,
Januari 7, mwaka huu, Rais Kikwete pamoja na mambo mengine, alihoji
uamuzi uliomwengua katika nafasi ya ubunge Dk Kafumu kwa kigezo cha
kufanya kampeni kwa kutumia ujenzi wa daraja hilo.Rais Kikwete alihoji mantiki ya uamuzi huo
wakati ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mambo yaliyopo kwenye Ilani ya
CCM ya2010–2015.Akizungumzia kauli hiyo, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law
Society (TLS), Francis Stola alisema hukumu hiyo ilikuwa sahihi kwani ni
makosa kwa kiongozi wa Serikali kutumia jukwaa la kampeni za kisiasa
kuzungumzia masuala yanayohusu utendaji wa Serikali akisema kufanya
hivyo kunaweza kutoa ushawishi kwa wapigakura na kuvuruga mwenendo wa
uchaguzi by http://www.mwananchi.co.tz
powered by nuhu85
No comments:
Post a Comment