MAKUNDI maalumu jana 10-01-2013 yaliendelea kutoa maoni yao kwenye mchakato
wa Katiba Mpya, huku DP kikipendekeza Rais aapishwe baada ya siku 90
tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Mbali na maoni hayo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti
wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila, makundi mengine;
wakulima, wafugaji, wanahabari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) nayo
yalijitokeza kutoa moyoni. Mtikila alisema kipindi hicho cha siku 90 kitatoa
fursa kwa watu wanaotaka kuwasilisha pingamizi dhidi ya ushindi wa Rais
mteule kufanya hivyo, kabla ya kuapishwa.
Alisema pingamizi linaweza kufanyiwa kazi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa taifa linapata kiongozi halali mwenye ridhaa ya wananchi. “Pia tunataka kinga ya Rais ikome pale anapomaliza muda wake wa uongozi, kama alifanya makosa yoyote ya jinai aweze kushtakiwa ili kujenga nidhamu ya uongozi katika ofisi ya umma. Utaratibu wa kumwondoa madarakani uimarishwe asisubiriwe hadi amalize muda wake wa uongozi.”Alisema kuwa Katiba ya nchi inapaswa kuwa mali ya wananchi wenyewe ili watawala wasijihusishe katika kuwaundia wananchi Katiba kama ilivyo kwa mchakato unaoendelea sasa wa kupata Katiba Mpya.
story by mwananchi magazine and powered by XI

No comments:
Post a Comment