Mbali na mjadala ndani ya jamii kuhusu
mustakabali wa ATCL, pia viongozi serikalini kwa nyakati tofauti nao
wamekuwa wakitoa ahadi za kufufua na kuimarisha ATCL iweze kutoa huduma
zake ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa enzi za uongozi wa Baba wa
Taifa, Hayati Julius Nyerere.
Ni jambo la aibu na kusikitisha kwamba kama
taifa lenye rasilimali zote ambazo nchi imebarikiwa kuwa nazo,
tumeshindwa kabisa kufufua ATCL na hasa pale ahadi lukuki zinapotolewa
bila ya kutimizwa.
Maoni yetu leo yanazidi kusisitiza kwamba
ndoto ya kufufua ATCL itimie ili tuweze kuwa na Shirika la Ndege.
Tunasema hivi kwa sababu sifa ya kuwa na Shirika la Ndege ni kuwa na
ndege za kutosha na kutoa huduma hiyo ya usafiri wa anga bila matatizo.
Tofauti na hivyo, tutaendelea kudanganyana kwamba kuna Shirika la Ndege
nchini wakati hatuna.Ndiyo maana taarifa za kwamba umoja wa
wafanyabiashara wa Oman wapo katika mchakato wa kukamilisha uwekezaji wa
Sh160 bilioni kwa ATCL zinaongeza matumaini kuwa huenda nchi ikarejea
kuwa na Shirika la Ndege.
nuhu85
No comments:
Post a Comment