UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa saratani ya shingo ya
kizazi, inasababishwa pamoja na mambo mengine na ngono kama ilivyo kwa
ugonjwa wa Ukimwi, madaktari bingwa wa magonjwa ya maradhi hayo
wamesema.
Hayo yalielezwa na daktari bingwa wa uchunguzi wa
magonjwa katika Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa.
Madaktari hao wametaja mambo mengine yanayoweza
kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye
mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa na wapenzi wengi,
kusafisha sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa mara nyingi.
Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa mwanamke kuzaa bila kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto wanne.
Dk
Mwakyoma alisema saratani ya shingo ya kizazi inatokana na aina 40 ya
virusi, aina mbili ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia ya ngono...
“Human papilloma virus (HPV) Squamos cell carcinoma kirusi namba 16 na
Adenocarcinoma namba 18, ni kati ya virusi 40 vinavyosababisha saratani
ya kizazi na vyenyewe vinachangia tatizo hilo kwa asilimia 70.”
Alisema saratani ya uzazi ndiyo inayoongoza
ikilinganishwa na nyingine nchini na asilimia 80 ya wagonjwa,
wameambukizwa kwa ngono.
“Saratani hiyo husambaa kwa ngono kutoka mwanamke
mmoja kwenda kwa mwingine. Mwanamke mwenye saratani ya kizazi akifanya
ngono, mwanamume huchukua virusi na kumwambukiza mwingine atakayefanya
naye ngono,” alisema na kuongeza:
“Wagonjwa wengi na wale ambao tayari wana
maambukizi, wamekuwa wakikutwa na virusi hawa wa aina mbili ambao
wamekuwa wakienezwa zaidi kwa njia ya zinaa. Inawezekana mwanamume akawa
ametoa kirusi kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.”
“Hata hivyo, kuna wanaume ambao tayari wameshakuwa
na maambukizi ya HPV wanatembea na virusi, hawa tunawaita (high risk
sexual male patner) wanaume hawa utakuta kila akioa mke anakufa kwa
saratani ya shingo ya uzazi, lakini kamwe virusi hao hawawezi kumwathiri
yeye.”
nuhu85
No comments:
Post a Comment